Na Derick Milton, Simiyu Siku chache baada ya kuripotiwa taarifa ya Mama Zawadi Sayi Abdallah mkazi wa Kidinda Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kudai kuwa alijifungua mapacha lakini akapewa mtoto mmoja. Serikali imeingilia kati tukio hilo na kueleza kuwa utafanyika uchunguzi wa kina ambao utavihusisha vyombo vya kiuchunguzi…